massawe japanni

Jambo Massawe: Bwanangu alikuwa ananyemelea auntie yake

Katika kipindi cha Jambo Massawe, chochote chaweza tokea, aidha kiwaache wengi na mshangao, furaha au pia huruma.

Hivi majuzi, mwanadada kwa jina Sylviah alipiga simu na kufichua jinsi mumewe alivyokuwa aki hanya hanya nje. Cha kushangaza ni kuwa mamake mdogo (shangaziye) ndiye alikuwa mpango wa kando.

Jambo Massawe: Nimefunga bibi, hawezi lala na mwanaume mwingine

Kulingana na mwanadada huyo kutoka Mt. Elgon, hajawahi guza simu ya bwanake kwa kipindi cha miaka sita ndani ya ndoa na pindi tu alipoguza alichokiona hakitatoka akilini hivi karibuni.

Alidai kuwa alichukua jukumu la kumpigia simu yule mwanadada na hapo ndipo alipogundua kuwa mumewe alikuwa na uhusiano na shangaziye.

Jambo Massawe: “Nilimkulia sister yangu bwana”

Soma usimulizi wake:

Yaani mimi mzee wangu nilimgundua yaani nilikuwa namshukushuku.Kushika tu simu yake, yaani nilipata maajabu maajabu nilipata messages walikuwa wana chat. Yaani nimekaa miaka sita kwa ndoa bila kushika hiyo simu yake lakini kushika tu siku moja, yenye nilipata akili karibu iruke.

Walikuwa tu wana chat; Mambo? poa. Aki babe umeamka aje? Utakam saa ngapi? eh! Aki kumpigia ni mamangu mdogo hata tumekosana!

Aki nilienda kumuuliza auntie yangu akaniambia alikuwa wangu zamani kabla uoleke, sasa nafikiria tu venye nitafanya hata nimenyamaza tu.

Skiza uhondo kamili.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments