massawe japanni comeback

Jambo Massawe: Bwanangu alinifukuza na akaoa dadangu (AUDIO)

Je mume wako akikufukuza na kuoa dadako utahisi vipi? Je waweza wasamehe kweli?

Akizungumza katika kipindi cha bustani la Massawe, Mama Chwele ni mmoja wa wanawake wanaopita masaibu hayo kwani alisimulia jinsi mzee wake alimfukuza pamoja na watoto wanne na kuoa dadake mkuu.

Isitoshe, wawili hao walipo oana walitorokea nchi jirani ya Uganda na hajawahi zungumza nao tangia mwaka wa 2011.

Bustani la Massawe: I have been smashing my boss’ wife for the last 6 years

Mungu naye alimbariki mama Chwele na bwana mwingine ambaye naye mabibi zake walikuwa wamemkimbia. Wawili hao walipendana na yule bwana akachukua wale watoto kama wake na huwa anawasomesha bila ubaguzi.

Soma usimulizi wake, kisha uskize kanda ifuatayo.

Mimi nilikuwa na mke wa ndoa ambaye tulioana tukiwa virgins. Tukazaa naye watoto wanne halafu tukawachana, akaja akaoa dadangu mkubwa nikawachana naye na akanifukuza na watoto, hata sahii hawezi shughulikia watoto lakini niko kwa ndoa ya pili.

Nikamwachia na hatujawahi kutana tangia mwaka wa 2011 mpaka sahii. Sasa wakatoroka na mzee hadi Uganda mimi nikaenda Nairobi nikaona maisha ya maid siwezi na nikarudi nyumbani. Nikapata mwanaume mwenye naye bibi alimuacha, nikamkubali naye akanikubali na mzigo wangu.

Nina watoto wanne, kijana amefanya form four, wasichana wawili last born na second last wako form two, huyu mwingine ako na shida tu ya kidunia sasa yeye ako tu nyumbani.

Lakini huyu mzee mwenye niko naye sahii, walahi namwombea mungu ampe miaka mingi kwa sababu anasomesha watoto wenye sio wake na sijawahi zaa nayewatoto.

‘I can’t support crap if it’s dirty, I won’t play it’ Massawe explains why she attacked Khaligraph

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments