massawe.J

Jambo Massawe: Nafikiria kumnunulia dada ya mke wangu shamba

Jamaa aliwaacha waskizaji wa Radio Jambo vinywa wazi alipokiri kuwa amekuwa na mpango wa kando na dadake mkewe kwa mda wa mwaka mmoja.

Huku akisumilia masaibu yake katika kipindi cha Jambo Massawe, mkewe ndiye aliyemleta mwanadada yule kwao nyumbani nao wakaanza uhusiano bila mkewe kujua, isitoshe, mwanadada yule ni mja mzito sasa hivi.

Jambo Massawe: Rafiki ya mume wangu alinitoa kwangu na kunioa

Alikiri kuwa mapenzi kati ya wawili hao yalinogeshwa pindi tu mkewe alianza ‘ujanja ujanja’ kwa nyumba na isitoshe anapangia kumnunulia shamba baada ya kumfungulia akaunti kwa benki.

Soma usimulizi wake.

 

Account nina mbili moja ni ya dada ya bibi sababu bibi yangu hanipeleki vizuri, sasa nimefungulia dadake kwa sababu niliona ana ujanja ujanja nami nikaamua nipate second party.

Dadake ananipeleka vizuri hata nafikiria kumnunulia shamba nimuoe. Mimi na dadake ni wapenzi kwa mda wa mwaka mmoja sasa, yeye ndiye alimleta kwa nyumba na mapenzi ikawa moto kwa nyumba.

Sahizi ananiamba ana dalili nikama ana mimba lakini hatujaenda kuangalia.

Nimemkombolea nyumba hizi pande za Kitengela na bibi naishi naye Syokimau. Sasa nikitoka Gari mapema stage ya kwanza ni huko halafu ikifika saa tatu naelekea kwa bibi.

Jambo Massawe: Bwanangu alinipea notice nihame

Pata uhondo kamili.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments