Jambo Massawe: "Nilimkulia sister yangu bwana"

Mwanadada kwa jina Anne alipiga simu akikiri bila aibu kuwa 'alimkulia' dadake bwana.

Kulingana na Anne aliyepiga simu katika kipindi cha Jambo Massawe, alisema yote yalianza wakti dadake alimuacha kwa nyumbani eti ampikie bwanake chakula. Hapo ndipo bwanake alipoanza kumyemelea huku akidai kuwa chakula chake ni kitamu kuliko cha mkewe.

Anne naye hakutupa mda kwani alitaka kuchovya asali ya dadake ili naye afurahie.

Soma usimulizi wake.

Mimi nimeshalala na bwana ya sister yangu. Sister yangu ananiwachia bwana mimi nimpikie, bwana akasema napika vizuri kuliko bibi yake.

Bwana akaninyemelea nikashtukia tushalala lakini sister yangu hakujua. Mimi niliingia box nikasema wacha niskie vile sister yangu anaskianga. Kama bwana ametaka nampea tu, lakini nilishaomba mungu msamaha kitambo.