Stori yake James ni ya kuhuzunisha kwani yeye ni muadhiriwa wa unyanyasaji ndani ya ndoa. Kulingana na James, mkewe kwa ushirikiano na askari wa polisi walikuwa wanampiga mbele ya watoto wake, wanamfunga kwa pingu kisha wanalalia kitanda chake cha ndoa.
Anasema kuwa shida zote zilianzia pindi tu walipojaliwa mtoto wa kwanza baada ya kungoja kwa miaka saba.
Mkewe alitoweka nyumbani na kumuachia mtoto wa miezi mitano ambaye hakuwa amemaliza kunyonya, bila sababu yoyote.
Watu wengi hufikiria kuwa wanawake pekee ndio huteswa na kudhulumiwa kwa ndoa, la, wanaume huogopa au kuona aibu.Hayo yote nimepitia kwani niliwachiwa mtoto akiwa na umri wa miezi saba na sasa nimemlea hadi amefikia miaka kumi na tatu. Mimi kwanza mke wangu alikataa kumnyonyesha mtoto wetu na kutoweka.
Baada ya mke wangu kutoweka ilibidi nimtafute kwa ushirikiano na wazee wa kanisa kwani mimi ni mchungaji na sikutaka aibu kanisani.
Cha kushangaza ni kuwa katika ndoa ya miaka 17, mkewe aliondoka mara kumi na kila mara alikuwa anabeba kila kitu kwa nyumba na kuwacha watoto bila hata sababu, licha ya kuwekewa biashara la duka na mumewe.
Alishikana na askari fulani ambaye alikuwa anakuja, ananifunga pingu ananipiga kisha analala kitandani mwangu mbele ya watoto wangu. Bibi yangui naye anachukua mwiko na kunipiga.Yule askari kisha ananipeleka katika kituo cha polisi na ananiandikia kuwa nimefanya kosa la kuvuruga amani nyumbani mwangu mbele ya watoto.
Anasema mkewe alipoenda Mombasa alibadilika na kuwa mnyama zaidi kwani alikuja na nguvu za giza na kuwa alikuwa anajipuliza marashi mengi sana. Isitoshe, aligeuka na kuwa kama mwanaume wa ile nyumba na alikuwa anamuamrisha ampikie chakula.
Ni si hayo tu kwani usiku bwana James alikuwa anahisi ni kama kuna watu ambao wanakanyanga paa la nyumba na ilibidi anyenyekee. Punde tu alipoanza kuomba kwa bidii, nguvu zile za giza zilididimia na hapo akaamua kuanza maisha upya.
James alisema kuwa siku ambayo aliamua amefika mwisho wakati alimuamrisha yule askari polisi amchukue mkewe kama mke wake. Hapo walijipanga na wakachukua kila kitu kwa nyumba na kuwaacha watoto pekee yao.
Hivi sasa yeye ni mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la sauti ya wanaume na watoto.
Wale watu wanaoumia sana katika ndoa ni wanaume kwani korti huskiza wanawake kuliko wanaume.