Janet Mbugua aeleza A-Z masaibu ya kuitema Citizen, asema sio dili freshi

Mtangazaji na msomaji habari Janet Mbugua amefunguka A-Z kilichofanya kuitema runinga ya Citizen.

Nyota huyu wa utangazaji aliwaacha mashabiki katika hali ya sintofahamu baada ya kupotea ghafla kwenye kioo cha runinga hii.

 Akisimulia katika kipindi kinachoendeshwa na Betty Kyalo, Janet amesema kuwa sababu kuu ya kuitema runinga hii na pamoja na kutenga wakati kumlea mwanawe na kuwa karibu naye.

https://www.instagram.com/p/B4E09cZHeas/

Janet Mbugua alikuwa akikana taarifa potovu zinazoendeshwa kuhusu kutoka kwake kwenye kituo hiki.

Taarifa zilikuwa zinahoji kuwa huenda nyota huyu aliitema runinga hii na kujiunga na shirika la kimataifa la habari.

Ina maana kuwa mwanadada huyu aliona kuwa hayupo karibu na mwanawe hivi ni sawa atenge wakati wa kuwa naye.

Janet anasimulia hapa jinsi alimkosa mwanawe,

https://www.instagram.com/p/B2ghHOvH61M/

“Sijui, nilikuwa napitia mengi wakati nilichukua hatua moja nyuma, nilikuwa nimechoka na nilikuwa nimeifanya kwa miaka 10. Kwa kweli sikuwa na uhusiano na Huru, na kuna siku ambayo nilijaribu kumkumbatia na akarudi nyuma," Janet

Mapenzi ya Janet kwa mwanawe yalichangia kuacha kazi kama anavyomsimulia,

"Hakuwa ananifahamu, kwa sababu kijakazi wangu alikuwa amefanya kila kitu. Kwa hivyo nikapanga mapato yangu kwa miezi sita na kuhakikisha yalikuwa sawa na kupanga miradi ambayo yangenisaidia kwa miaka miwili," alikariri Janet.