janet otieno

Janet Otieno Asimulia Jinsi Alivyomgeuza Weezdom Kutoka ‘Kijana Wa Mkono’ Hadi Kuwa Msanii

Msanii wa nyimbo za injili Janet Otieno pamoja na msanii chipukizi, Weezdom wana wimbo mpya kwa jina ‘Amka Ucheze’ ambao tayari umeanza kukita mizizi mioyoni mwa mashabiki wake kote nchini na duniani kote.

Kulingana na Bi. Otieno, wimbo huo unazungumzia namna wakenya na binadamu kwa jumla wanapaswa kumchezea mungu kwa wakati wowote; Ukiwa ni wakati wa dhiki, majonzi, hasira hata furaha kwani mungu pekee ndiye suluhisho wa yote.

Cha kushangaza ni kuwa msanii Weezdom aliwahi mfanyia msanii Janet Otieno kazi ndogo ndogo ambazo zilipelekea yeye kubandikwa ‘Kijana wa mikono’.

Mojawapo ya kazi ambazo Weezdom amewahi mfanyia Janet na kumsaidia katika uzalishaji wa video ya wimbo wa ‘Uniongoze’ ambapo yeye ndiye aliyepanga na kuwasha mishumaa zaidi ya mia mbili ambazo ziko kwa video hiyo.

“Weezdom nimekutana naye kama 2013 mwisho na alikuwa anafanya kazi katika projects zangu nikiwa na shoot video nilikuwa namuona akifanya kazi za mikono.” Alieleza Janet.

Kama kuna wimbo wangu mmoja unaitwa niongeze, nilikuwa na shoot usiku na set up ilikuwa inahitaji mishumaa na nakumbuka nikimuona mara ya kwanza yeye ndiye alitumwa zile mishumaa na akaja kuzipanga.” Aliongeza maneno ambayo Weezdom mwenyewe alithibitisha katika mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji Annita Raey.

Tizama kanda ifuatayo.

Photo Credits: Janet Otieno

Read More:

Comments

comments