63dc2d8b_3e15_478e_94e8_eabc912c622b__1574088839_53091

Jasiri aliyeingia na genge lake katika eneo la mkasa wa bomu 1998

Kanoga amesimulia Massawe jinsi yeye na wenzake waliingia katika eneo la mkasa wa bomu kutafuta pesa.

Bomu hiyo ililenga ofisi za ubalozi wa Marekani mwaka wa 1998.

Aidha, jama huyu amesimulia jinsi makali ya mvua ya Elnino yalivyompata pabaya na jeshi lake.

Wengi wa marafiki wake walipoteza maisha katika eneo hili la mkasa wa bomu.

Masaibu ya Babu Owino, ataja sababu za mahasidi kutaka kumtoa uhai

 Wilson ambaye kwa sasa amebadilika alikuwa na genge lake la vijana wanaorandarada mitaani wakati huo.

“Wakati huo tulikuwa street children,tuliingia huko wakati huo bomu ilipuka kutafuta pesa na kupora mali…”

Aidha, njama na njaro za kufuata mtu hadi benki ili kujua ni kiasi gani cha pesa alikuwa mjuzi wa hilo.

Baadaye angekupaka rangi ili uweze kuonekana na chokora wale wengine wakufuate.

“Ningekupaka rangi baada ya kuona pesa umetoa. Ama nakufuata nijue kwako ili nitume wezi waje kukupora…”

Kanoga alipoteza babake na umri mdogo sana,

Sumu iliyowakosa Shanice na Michael, mamake Joyce Syombua asimulia

“Babangu alikufa nikiwa mdogo, mama aliniacha akaolewa pengine na kwa sasa hatuna uhusiano wa karibu na ma-sister…”

Huku akihesabu aina za dawa alizotumia, Kanoga ana kovu la jeraha kichwani alilopigwa shoka na genge la wezi.

“Nimetumia cocaine, brown sugar na nikauza dawa za kulevya Kencom…”

Kanoga amesema baadaye alikuja kubadilika na kuwa mwema.

 

Photo Credits: FILE

Read More:

Comments

comments