Jayjay Okocha asimulia alivyobaguliwa Ujerumani kwa kuwa mweusi.

Aliyekuwa mshambulizi wa timu ya taifa ya Nigeria Jayjay Okocha amesimulia jinsi alivyo waadhibu wajerumani waliombagua kwa kuwa mweusi. Okocha alikuwa maarufu kwa chenga zake za kimaudhi zilizo waacha wengi wakiziramba nyasi uwanjani.

"Nilipoenda Ulaya, taifa ya kwanza ilikuwa Ujerumani. Nilipofika huko ndipo niligundua kwamba mimi nilikwa mweusi. Ubaguzi wa rangi ulikuwa wa hali ya juu sana. Sikuwa na njia ya kujitetea ila kuwaonyesha umahiri wangu wa kuchenga na kufunga magoli. Nilianza kuwapiga chenga ilikulipiza kisasi," Okocha alisimulia.

Taifa la ujerumani ni moja kati ya mataifa yanayoongoza kwa ubaguzi wa rangi. Kevin Prince boateng, Anthony Ujah pamoja na leon Balogun ni baadhi ya wachezaji waliopitia wakati mgumu wakicheza mechi za ligi kuu ya Ujerumani msimu uliopita.

Suala la Ubaguzi wa rangi limekuwa likiongezeka kila uchao huku wachezaji waafrika pamoja na wachezaji wenye asili ya kiafrika wakiwa waadhiriwa wakubwa.

Kwenye mechi dhidi ya Eintracht Frankfurt na Kalsrhue, Okocha alisimulia jinsi walinzi wa kijerumani walivyomfananisha na tumbili. Hatahivyo, Okocha alifunga goli kwa kuwala  chenga za kimaudhi walinzi hao pamoja na mlindalango wao,"Oliver Khan" nakuipa timu yake ya Frankfurt ushindi.