Je BBI itaporomoka?Raila awaambia maseneta wa ODM kukataa mfumo wa ugavi wa mapato

BBI
BBI
Mwafaka wa BBI  huenda upo mashakani baada ya  washirika wa kisiasa wa kiongozi wa ODM Raila Odinga kudai kwamba kuna njama ya kumtema .

Wandani wa Raila wanadai kwamba wenzao katika upande wa Jubilee wameanza kuwatolea vitisho ili kushawishi maamuzi yao kuhusu mfumo unaotumiwa kugawa mapato kwa serikali za kaunti baada ya kuhusisha kura ya kupitisha mfumo huo na hatima ya mwafaka wa  BBI .

Wamedai kwamba washirika wa rais Kenyatta  wamekuwa wakiashiria kwamba mchakato mzima wa BBI ni mradi wa Raila . Raila na washirika wake hawajapendezwa na hatua ya kujaribu kutumiwa kwa vitisho hivo vya BBi ili kuwashurutisha wapitishe  mfumo mpya wa ugavi wa mapato ambao utapunguza kabisa mgao katika kaunti nyingi ambazo ni ngome ya Raila .

Mfumo huo mpya kulingana na  washirika wa Raila  ni njama ya kutikisa  uungwaji mkono wa Raila katika ngome zake  ili kuwafanya wafuasi wake kumgomea wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2022 .

“ Njama ni kumsalimisha Raila ili wampate mtu wanayemtaka . mfumo huu wa ugavi wa mapato utazua lalama kubwa zaidi kuliko inavyodhaniwa’ amesema mwanachama sugu wa ODM  .

Kwa mfano anasema maeneo ambayo yanafaa kupata mgao wa juu ndio yatakayopata ufadhiliw a chini na yametrengwa kwa muda mrefu .

Gazeti la The Star limesema Raila alifanya mkutano wa njia ya mtandao na   kamati ya usimamizi wa chama na kuafikia kukataa mfumo huo unaopendekezwa na serikali .

Hatua hiyo huenda sasa ikarejesha tena uhasama wa kisiasa kati ya Odinga na  Rais Uhuru Kenyatta ambao walikuwa wameafikia makubaliano ya kushirikiana .