Je Diamond na dadake Vanessa Mdee wanachumbiana? (PICHA)

diamondandmimi-727x1024
diamondandmimi-727x1024

Swali la kama kuna uwezekano kuwa msanii shupavu Diamond Platnumz na Mimi Mars ambaye ni dadake Vanessa Mdee wanachumbiana, limekuwa likiulizwa kwa mda sasa.

Hata hivyo, wawili hao wanawanyima mashabiki wao usingizi huku wengi wakiomba habari hizo ziwe za kweli.

Juzi, Diamond alichapisha Kanda ya wawili hao wakiogelea nyumbani kwake huku wakibugua vinywaji na wakijivinjari pamoja.

Video hizo zilisisimua hisia za wengi huku ikiwa wazi kuwa Kuna uwezekano wawili hao wanachumbiana.

Siku kadhaa zilizopita Mimi aliandika ujumbe akiashiria kuwa amepata kuonja mapenzi na hapo wengi wakajijazia kuwa yeye na Diamond wana uhusiano.

Mimi aliandika,

"Palipo na upendo hapana woga; naam, upendo kamili hufukuza woga wote. Basi, mtu mwenye woga hajakamilika bado katika upendo, kwani woga huhusikana na adhabu.”

‭‭1 Yohane‬ ‭4:18‬ ‭

#mimimars #chuggaqueen"

Zifuatazo ni baadhi ya ujumbe kutoka kwa mashabiki wao :

willy_dangote_

SIMBA ANAKULIA TYMING UKIJILES TU KIBENDI🤰😂.

babuallymsodoki

Mkubalie basi jamaa yetu 😁

mkil_indi

Dada Leo usiku ukikutana na mond mforce avae condom Mana tanasha,hamisa na zari unawaona wanavyohangaika na vifaranga

njowoka_junior

Kaka dayamondi amesema anakuelewa kinoma siso mashabiki wa WCB tumekubali kukukaribisha😁

ulu_ark

Sawa nasibu ujumbe umemfikia..

gucci_music_tz

Chibu ashakubeba usiwe na woga anazalifa afu anawaacha wewe atakuacha

Wawili hao bado hawajazungumzia uhusiano wao lakini ikumbukwe kuwa Diamond alisema kuwa yuko tayari kutafuta mpenzi atakayefunga pingu za maisha naye mwaka huu.

Hakikisha kuwa umesoma habari zetu kwani tutakupasha habari zote kuhusu wapenzi hawa wawili kila tunapozipata.