Je Mourinho atafufua fomu ya Wanyama? Wakenya watoa maoni (VIDEO)

training.jose.20nov.5
training.jose.20nov.5
Ni siku chache tu baada ya Mourinho kuteuliwa kama kocha mpya wa Tottenham Hotspur masaa machache baada ya Mauricio Pochettino kutimulia baada ya miaka mitano ugani White Hart Lane.

Mourinho aliregea kwenye ligi kuu ya Uingereza tena na timu tofauti kwani aliwahi kuwa kocha wa timu kama Chelsea na Manchester United, na ana kibarua kigumu kufufua fomu ya timu hii ambayo sasa iko nambari 14 baada ya mechi 12.

Wakenya nao wana matumaini kuwa nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama, ambaye hajakuwa akipata fursa ya kucheza msimu huu atapewa nafasi ya kuthibitisha kuwa bado ana makali.

Hata hivyo, wengi wao wanahisa kuwa mda wa Wanyama kama mchezaji wa kulipwa unadidimia na kuwa anapaswa kutafuta nafasi katika timu nyingine.

Katika kanda ifuatayo, tunapata maoni mbali mbali kutoka mashabiki wa soka kuhusu uteuzi wa 'special one' na kama ana uwezo wa kufufua Spurs.

Mechi ya Mourinho ya kwanza akiwa usukani atachuana na West Ham katika uga wa London, saa tisa unusu hii leo.