Je Mumeo Amekataa Kulala Kitandani Chenyu? Bi Gertrude Mungai Ana Mawaidha (AUDIO)

Getrude-Mungai
Getrude-Mungai
Je, unatatuaje swala la mumeo kuacha kulala kitandani na kufanya kiti kuwa kitanda chake? Annita Raey aliuliza.

Hili ni swala ambalo wanajambo waliomba lizungumziwe ili wapate fursa nzuri ya kujua jinsi ya kutatua shida zao za kindoa na kuwarudisha wanaume vitandani vyao.

"Kitu cha kwanza sidhani kwamba mwanamume anaweza kuja kwa nyumba na kuamua kulala sebuleni lazima kuna vijimambo vidogo vidogo ambavyo vimetokea na hawajaweza kujiweka wenyewe kama watu wazima ili kusuluhisha.

Na kunao wanawake wengine ambao hujitoa kwa chumba na kwenda kulala na watoto. Lakini baba mzima mwenye ndevu zako unaacha mkeo ndani ya chumba na unaenda kulala sebuleni, hata mfanyikazi atasemaje? Aliuliza Getrude Mungai.

Kitu kizuri ni mwanaume kuketi chini kama kichwa cha nyumba ni kuketi chini na kusuluhisha hayo. " Aliongeza.

Kulingana na wanawake wengi haswa waskilizaji wa Radio Jambo ni kuwa wanaume wengi wakilewa huwa wadhaifu kitandani ikifika ni tendo la ndoa na jambo hilo huwaudhi sana.

Bi Getrude alikuwa na mawaidha kwa wanaopitia hayo.

Unajua wakati wa ndoa kama bwana umemfunza kuwa akibugia pombe asije akalala kitandani, hilo sio jambo zuri kwani yeye sio mtoto na kama hiyo ndio starehe yake usimkashifu kwa sababu wewe hunywi." 

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be