Je, mwanaume atajuaje kama ana saratani ya matiti?

Breast-cancer-symptoms-in-men-Four-changes-in-the-nipple-to-watch-for-1278055
Breast-cancer-symptoms-in-men-Four-changes-in-the-nipple-to-watch-for-1278055
Je, mwanaume atajuaje kama ana saratani ya matiti?

Wengi wetu tumekuwa na dhana kuwa wanawake peke yao ndio wapo kwenye hatari ya kupata saratani ya matiti.

Ila wanaume wapo kwenye hatari hiyo ya kansa hii japo ni muhali sana.\

Ni visa vichache utaviskia vya aina hii hapa nchini japo kuna uwezekano vikatokea.

Ni vizuri kwa wanaume kuwa wanatembelea vituo vya ukaguzi ili kubaini hali yao ya kiafya.

Pale, daktari au wauguzi wataweza kuwafanunulia viashiria vya gonjwa hili sugu.

Siri kuu ya kupigana na saratani yoyote ni kupimwa mapema ili uanze matiabu ya awali.

Hii inazuia virusi hivyo kusambaa kwenye viungo vingine mwilini.

Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa katika mstari wa mbele kuhimiza watu kuhusu swala hili.

Maafisa wa afya wanahoji kuwa licha ya wanawake kuwa waathiriwa wakubwa wa aina hii ya saratani, wapo pia wanaume wanaopatwa na ndwele hii.

Mpaka sasa tumeshuhudia visa vya watu kufariki kwa sababu ya kansa.

Viongozi serikalini hawajasazwa nyuma na zimwi hili.