Gloria-with-pastor-Omba

Je ni ukweli mume wake Gloria Muliro alikuwa na mpango wa kando?

Ndoa ya Gloria Muliro ilipovunjika alimlaumu mume wake na kusema kuwa aliyekuwa mume wake alikuwa na mpango wa kando.

Muliro alisema kuwa alikuwa na uhakika kuwa mume wake alikuwa na mpango wa kando kwani rafiki zake walikuwa wanamwambia lakini alikuwa anajifanya kutoskia mambo yao.

Ripoti ya Sarah Cohen, Maelezo ya unyama aliyotendewa na Tob

 ‘Nilikuwa najua kuwa alikuwa na mipango ya kando. Rafiki zangu walikuwa wanakuja kuniambia lakini                nilikuwa najifanya sisikii mambo yao.”Gloria Alisema.
Hata hivyo, Kasisi Omba aliyekuwa mume wake Gloria Muliro alisema kuwa Gloria hakuwa na picha, idhibati na hata hakuna msichana yeyote aliyekuwa amefunguka waziwazi na kusema kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na yeye.
” Gloria hakuwa na picha, idhibati wala hakuna mwanamke yeyote aliyefunguka na kusema kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mimi, ” Omba
Zaidi ya hayo, Omba alisema kuwa hakuwa na mpango wa kando na hata hakuwa na sababu ya kumdanganya Gloria kimapenzi.
“Alikuwa anasema anachosikia kutoka kwa marafiki wake. Sikuchepuka na nilikuwa mwaminifu. Mbona niwe na jicho la nje? Alisema Omba.

Vilevile, Omba alipoulizwa ni somo lipi alipata alipokuwa kwenye ndoa yake na Gloria alisema kuwa wanawake wanafaa kuwa wanazingatia maisha yao na mume wao na si kusikiliza mambo ya watu kwani jambo hili linaweza kuharibu ndoa.

“Nimemuua. Sasa kujeni mniue,” Mshukiwa awapigia simu polisi

”Alichokuwa nacho Gloria kila mwanamke anacho. Wakati mwingine unafaa kuzingatia mume wako na si                kusikia mambo ya watu wengi kwani tabia hii itaharibu ndoa yako.” Omba

Baada ya ndoa yake Omba na Gloria Muliro kuvunjika, bwana huyu alioa mke mwengine na kwa sasa anaishi maisha mazuri na mke wake.

Gusa hapa usome hadithi za Sedellar Righa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments