Je, shirika la Sky News 'lilimuua' Cedric Shivonje? Picha waliotumia sio za Manyasi

Screenshot_from_2019_11_13_06_36_47__1573648777_75099
Screenshot_from_2019_11_13_06_36_47__1573648777_75099
Mamlaka ya gereza imebaini kuwa picha iliyotumiwa na shirika la habari la Sky News ni la Cedric Shivonje ambaye yuko hai.

Mamlaka hii imeitaarifu BBC kuwa picha iliyotumika ni ya Cedric.

Cedric alizuiliwa korokoroni tangu Agosti mwaka huu.

Hivyo basi ni dhihirisho kuwa shirika la Sky News 'limemuua' Cedric Shivonje kimakosa.

Je, iwapo familia ya Cedric itachukua hatua ya kisheria dhidi ya shirika hili mambo yatakuwa vipi?

Kizungumkuti kimetawala swala nzima la kubaini 'mtu' kwa jina la Paul Manyasi aliyefariki baada ya kujificha katika sehemu ya magurudumu ya ndege na kuanguka ilipokaribia kutua Uingereza.

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ kiliwatia wengi hofu kubwa.

Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Manyasi alikuwa akiishi Mukuru kwa Njenga viunga vya jiji na alikuwa na rafiki yake Partrick.

Patrick alisema kuwa Paul alikuwa na ndoto ya kuhama Kenya.