Je, Sonko alifichua kuugua Ukimwi kwenye hati za kiapo mahakamani?

MIKE SONKO 1
MIKE SONKO 1
Gavana wa Nairobi Mike Sonko alifichua katika hati za kiapo kortini kuwa aliugua virusi vya Ukimwi pamoja na magonjwa mengine.

Hati za kiapo mahakamani zilizowasilishwa na mkurugenzi mwendesha mashtaka ya umma DPP inaonyesha kuwa Sonko alidai kuwa anaugua ugonjwa huo na kutaka mahakama imwachilie ili anusuru maisha yake, miaka 18 iliyopita.

Sonko ambaye alikuwa gereza la Kamiti akisubiri uamuzi wa jaji Douglas Ogoti kuhusu ombi la kuachiliwa kwa dhamana Jumatano, aliugua na kukimbizwa hospitali ya KNH kulingana na mkuu wa mawasiliano yake, Elkana Jacob.

Kulingana na gazeti la Star, Gavana Sonko mnamo 2001, kupitia kiapo cha mahakama alidai kuugua virusi vya Ukimwi pamoja na ugonjwa wa kifafa.

Aidha, alidai kuwa alikuwa akiugua ugonjwa sugu wa kifua kikuu na maradhi ya vidonda kwenye tumbo lake. Hayo ni kulingana na hati ya kiapo mahakamani.

Mnamo 2001, Gavana Sonko aliongeza kusema kuwa alikuwa mwana wa mama pekee na ambaye aliaga dunia akiwa gerezani.

Kulingana na upekuzi wa gazeti la Star, hati za kiapo za Sonko tarehe 2/2/2001, akitetea ombi la kuachiliwa kwake huku akidai kuwa magonjwa hayo na hali yake ya kiafya ilihitaji utunzi na matibabu ya hali ya juu.

"Kwa sasa nimelazwa katika hospitali ya gereza na nafasi ya kupona ni finyu sana hivyo basi ninaomba kuachiliwa kwa ajili ya kwenda kujitafutia matibabu au kwa amri ya rais ya kuachiliwa huru wafungwa tarehe 12/12/200," Sonko alisema.

Hati hiyo ya kiapo iliwasilishwa katika mahakama kuu ya Nairobi.

Miezi mitatu baadaye, jaji wa mahakama kuu Samuel Oguk aliamuru Sonko kuachiliwa kutoka gereza kabla ya kumaliza kifungo chake cha mwaka moja kwa madai kuwa alikuwa anaugua virusi vya Ukimwi.

Siku moja tu baada ya kukamatwa, Sonko alipelekwwa hospitali ya kitaifa ya Nairobi huku madaktari wake wakisema kuwa ana maumivu  kwenye mpafu zake na shinkizo la juu la damu.