Je tiba ya Babu wa Loliondo iliponesha?

Bado mnamkumbuka Babu wa Loliondo? Jamaa ambaye alidai kuwa ana tiba ya magonjwa yote ikiwemo ukimwi kirusi ambacho ni tishio kubwa kwa kizazi cha sasa.

Miaka tisa iliyopita kulikuwa na msafara mkubwa wa magari, baisikeli, ndege hewani yote tisa, kumi ikiwa kupata matibabu kutoka kwa dawa aliyoitengeneza babu.

Umati mkubwa ulikusanyika nyumbani kwa babu ili angalau wapate tiba hilo, lakini je? walipona? Ni suala ambalo limeibua hisia mbalimbali humu nchini na pia maeneo kadhaa kule Dar-es-salaam Tanzania, huku wengine wakikashifu tiba ya babu kwa kutofanya kazi licha ya wao kusafiri kilomita kadhaa kupata tiba hilo huku wengine kwa upande huu wakidai kuwa dawa hiyo ya babu inaponya.

Ambilikiwe Mwasapile ambaye anafahamika vizuri kama Babu wa Loliondo, alisema kuwa ni Mungu alimuelezea jinsi ya kutengeneza dawa hiyo ili awasaidie watu.