Je, ubishi wa Magix Enga na Harmonize kisa UNO umefanya akamatwe na polisi?

magix2_e1575233224483__1575273477_55733
magix2_e1575233224483__1575273477_55733
Mtayarishaji wa nyimbo Magix Enga almaarufu kama Beat King ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi.
Magix amedhibitisha taarifa hizi kupitia akaunti yake ya Insta.
Katika video hiyo, Enga anasikika akiuliza maafisa hao “Mnanikamatia nini mazee kama wimbo ya Harmonize tayari iko YouTube."

Kulikuwepo na ubishi wa midundo ya ngoma ya Uno kati yake na mwimbaji wa Bongo Harmonize siku chache zilizopita.

Sio tu ngoma ya Uno ya Harmonize, Enga alikuwa bado ametishia kuifungia ngoma ya msanii wa Nigeria Olamide inayofahamika kama Motigbana.

"Olamide, pia wewe nakupatia wiki moja. Midundo yangu ni wiki moja, ngoma yako ina mwaka mmoja YouTube. Ila unaweza piga simu ueleze kabla wiki haijaisha." Alitishia mtayarishaji huyu.

Mtayarishaji huyu wa ngoma nchini Magix alitoa onyo kali kwa msanii yeyote anayeiba midundo yake.
Haijabainika kabisa kilichopelekea Magix kukamatwa.

Enga alikamatwa usiku wa Jumapili pamoja na mwenzake Maurice.

Je, kuna uwezekano Uno ya Harmonize ndio inasababisha kukamatwa kwa Magix Enga