Je, Uhuru anamzubaisha Raila huku akimuunga mkono Ruto?

Uchaguzi mdogo wa eneobunge la Kibra umeibua maswali juu ya mikakati ya mrithi wa Rais Kenyatta na ni nani anayemuunga mkono kikamilifu kati ya kiongozi wa ODM Raila Odinga na Naibu wa Rais William Ruto.

Wakati Rais amekuwa thabiti katika mazungumzo yake kwa umma kwa kuunga mkono wito wa maridhiano wa Handshake baina yake na Raila,  wafuasi wa Ruto  nao wanasisitiza Rais bado anamuunga mkono  mtu wao.

Uchaguzi mdogo wa Kibra umekuwa kikwazo kikuu kwa azma ya Rais ya kushikilia wahusika hao wawili kwa hatua ya kimikakati ya kutotatiza uwasilishaji wa Ajenda zake kuu ya Nne.

Baadhi ya wafuasi wa Uhuru kati yao ni Seneta wa Nairobi John Sakaja awali akisema kwamba Jubilee haingeteua mgombea wa Kibra, Ruto alimchagua mwanasoka Macdonald Mariga na kuhakikisha kuwa yeye atakabilaina na mteuzi wa Raila katika chama cha ODM  Imran Okoth.

Mnamo Septemba 18, mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino  alimtuhumu Rais kwa kumteua Mariga kuwa mwaniaji wa chama cha jubilee.

Owino alimtuhumu Rais kwa kusaliti wito wa maridhiano kwa kumuunga mkono kiungo  cha kati wa zamani wa Inter Millan ambaye anawania kwa tiketi ya Jubilee.

"Baba lazima awe mwangalifu sana kwa jambo hili linaloitwa  Handshake. Hakuna matunda hadi sasa. Hatuwezi tukazubaishwa mara mbili. Rais Uhuru lazima awe mkweli kwa kuhusiana na Handshake," Owino alisema katika machapisho yake Facebook.

"Hatuna budi kuambiana ukweli wakati kusudilao ni kuwadhalilisha. Kamwe Jubilee  haitashinda Kibra. Niko tayari kurudi kwenye kichaka."

Siku ya Jumapili wakati  akiwa katika kampeni zake, Mariga alidai Rais  alimuita ili kudadisi  maendeleo yake.

"Ninyi nyote mnamjua aliyenivalisha kofia ya Jubilee? Nilialikwa pamoja na wabunge wa Jubilee. Tulikaa chini na Rais na aliniambia wakati wa kampeni zangu nilipaswa kuzungumza na jamii ya Akiguyu huko Kibra na wataniunga  mkono," Mariga alisema.

Siku moja tu baada ya Mariga kukutana na Uhuru katika Ikulu, mbunge mteuliwa Maina Kamanda alikutana na Raila na kutangaza kwamba atampigia kampeni Imran.

Katibu mkuu wa utawala Rachel Shebesh alikutana na viongozi wa wanawake wiki mbili zilizopita na alidai kuwa Rais aliviziwa na kwamba hakunuia  kumuunga mkono Ruto.

"Ana mdomo wake. Je! Umesikia akisema anamuunga mkono Mariga?", Alisisitiza Shebesh ambaye anafahamika kuwa karibu na Uhuru.

"Rais anafahamu wazi kuwa mtu yeyote atakayeingilia kati Naibu Rais au Raila itakandamiza juhudi zake za kutoa huduma kwa taifa," mhadhiri wa chuo kikuu Macharia Munene alisema.

Munene, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Merika, aliiambia Star hiyo Rais anatembea kwa laini ya kisiasa.

"Rais huwa kimya sana wakati Ruto na Raila wanagombana kisiasa. Kwa mfano huko Kibra, Rais anajaribu kufurahisha kambi zote mbili, kwa sababu matokeo yoyote hayana maana kwake "alisema.

Kwa upande mwingine Rais ameonekana akifanya kazi na Raila hata alisherehekea siku ya kuzaliwa ya Raila huko Mombasa mnamo Januari 7 na kumtembelea kiongozi  huyo wa upinzani nyumbani kwake Bondo.

Tofauti na hapo awali wakati Kenyatta na Ruto walihudhuria mikutano kwa pamoja, hata walivaa mashati sawa na tai zinazofanana pia, Rais amekuwa akiendesha shughuli zake peke yake na inasemekana hashauriani na DP kama vile alivyofanya katika kipindi chake cha kwanza.

Kwa upande mwingine Rais ameonekana akifanya kazi na Raila hata alisherehekea siku ya kuzaliwa ya Raila huko Mombasa mnamo Januari 7 na kumtembelea kiongozi wa Upinzani nyumbani kwake Bondo.

Rais amewatupa wanasiasa hao wawili katika machafuko zaidi na baada ya uhusiano wake wa kisiasa na wa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi kuibuka.

Walio karibu sana na Rais waliambia Radio jambo kwamba Rais amekuwa akizungumza na Mudavadi, rafiki yake tangu utotoni, mara kwa mara na hata akamtia moyo aendelee na jukumu la kiongozi wa upinzani.

Wakati wa hafla ya Kenya  Open Golf huko Karen mapema mwaka huu, wawili hao wanasemakana kuwa na mkutano wa masaa mawili.

Kiongozi wa Ford Kenya Moses Wetang'ula anasema Rais anaweza  akawashnagza wengi  kwa kuwa hakuna ajuaye mipango yake.

"Hatujui zaidi kuhusu Hanshake. Rais ni huenda si mwaminifu kwa Ruto au Raila.  Wote hao Ruto wanafanya kazi gizani, wote wawili wakijaribu kutabiri hatua zitakazofuata,"  Wetang'ula alisema.

Mbunge wa Starehe Charles Njagua alisema Rais hayuko katika hali yoyote mtanziko kwani ameonyesha kumuunga mkono Mariga.

"Rais amekuwa wazi ni nani anamuunga mkono. Ni kambi nyingine ambayo imepotoshwa," Njagua alisema.

Wakati Uhuru ameepuka kufanya kampeni ya hadharani kwa Mariga kwa uchaguzi mdogo wa Novemba 7 kama vile alivyofanya  katika  uchaguzi mdogo wa Wajir Magharibi, yeye hajapinga madai kutoka sehemu ya viongozi wanaopinga Ruto kuwa Rais anauunga mkono ODM

Mbunge wa Belgut, Nelson Koech alimrai Uhuru "aiweke nyumba ya Jubilee sawa", akisema kimya chake "kimeibua mtazamo kuwa yeye ni Rais asiye na uwezo."

"Ijapokuwa ninajua kuwa Rais anamuunga mkono  Mariga, itakuwa kwa faida nzuri sio tu kwa Jubilee bali kwa nchi, kwake au kupitia idara yake ya mawasiliano aweke bayana kuhusu mtanziko uliopo," alisema.

Mbunge wa Dagoretti Kaskazini John Kiarie alitupilia mbali madai kwamba Uhuru hajamuunga mkono ipasavyo Mariga huku akisema kwamba  Rais ana imani kwa mwanasoka huyo.

"Jubilee ina mgombeaji mmoja ambaye alitawazwa na Rais Uhuru Kenyatta mwenyewe. Wale wanaosema Mariga sio mgombeaji wa Jubilee ni wale waliokatailiwa  kisiasa  na walishindwa katika uchaguzi uliopita na wana kinyongo na DP," Kiarie alisema.