Je uliolewa kwa sababu ya mapenzi au shida? Wakenya wafunguka

ndoa marriage
ndoa marriage
Ni dhahiri kuwa, humu nchini wasichana wengi hawako kwa ndoa kwa ajili ya upendo au mapenzi yao kwa waume zao, ila wengi walilazimika kuingilia ndoa ili kuepuka ufukara.

Isiroshe kinadada wengi walilazimishwa na wazazi wao waolewa ili waweze kuokoa familia zao kutoka kwa uchochole. Hii ni kwa sababu familia yao hunufaika na fedha au mahari kwa njia ya mifugo na zawadi zinginezo.

Na hali ngumu kama hizi ndizo hupelekea ndoa nyingi kuvunjiva zikiwa changa au pia unapata familia nyingi zinaishi kuzozana kwani, hakukuwa na msingi wa mapenzi au hata urafiki.

Basi tuliamua kuwauliza wanajambo iwapo wako kwa ndoa kwa sababu ya hali ambazo hawangeepuka, au wamo hapo kwa ajili ya mapenzi ya ukweli.

Hata hivyo majibu tuliyoyapata ni ya kushangaza na utaelewa mbona visa vingi hujulikana au kutibuka wakati wa patanisho.

Soma baadhi ya majibu yao.

Charles Ochieng: Hakuna kitu mbaya humu dunia Kama shida haijuwi mdogo wala mkubwa masikini ama Tajiri mwimbaji alisema na pia Hakuna kitu mbaya Kama kuolewa juu ya shida Mwanaume uchukua hio advantage Sana kukudhulumu

Dorcas: Sababu nilipata mimba bure!

Njuguna: Sio mapenzi wala shida Bali aibu juu niko mja mzito wakati huo....Sinai iko ndani

George Gitonga: Kwani iko kuoa mm ni kukalishana masiku ziende anyway miaka ya kuoa bdo

Robin Onyando: Mtu anaolewa sababu ya kusaidiana kwa njia mbalimbali nikiwa nrb githurai44 naskiza na Mke wngu happy Teresa watoto Nelson onyando glory onyando na cleophas salano

Fred yule:  Massawe vipi, watu huolewa kwa sababu miaka inawachenga