Je umehitimu kuwa Sponsor? Usimpe msichana nauli ukitaka uroda

Je, ushawahi kumtumia mrembo nauli aje kwako na ukaambulia patupu?, ole wako mbunge wa Suba North Millie Odhiambo ana ushauri kwa vijana wa kiume walio na mazoea ya kuwatumia warembo nauli.

Millie anawaonya wanaume dhidi ya kutumia vidosho nauli, anasema “usimtumie msichana nauli yoyote”.

Soma pia...

Ushauri wake unajiri wakati wanaume wamekuwa wakilalamikia hatua ya wanawake “kula nauli” na kisha kukataa kupokea simu zao au tu kusalia kimya licha ya kupokea pesa.

Akizungumza katika jarida moja la humu nchini, mbunge huo alisema;

MBONA UMTUMIYE PESA KWANZA? KATIKA DUNIA HII YENYE USAWA, WACHA KILA MTU AJILIPIYE NAULI. JILIPIYE NAULI UKIENDA KUMTEMBELEA MWANAMUME NA UWACHE MWANAMUME PIA AJILIPIYE AKIJA KUKUTEMBELEA. UKIWA MJINGA SANA KUMTUMIA MREMBO NAULI, USILALAMIKE AKIKOSA KUJA KWA SABABU WEWE SIO MWANAMUME, WEWE NI MASHINE YA ATM NA ATM HAZILALAMIKI.UHUSIANO WA KIMAPENZI HAUFAI KUINGIZWA PESA NA MWANAMUME AU MWANAMKE.

Ukitaka kurusha roho kaka wacha mwenyewe ajilipiye nauli.

Soma pia...