Je, unafahamu jina linalotumiwa kuita pesa mtaani kwako?

Unafahamu lugha ambayo inatumiwa sana sana na vijana mitaani wakati pesa inatumika kuuza au hata kununua bidhaa mbali mbali?

Naam basi majina hayo ni vizuri kuyajua usije ukachanganyikiwa.

1.NGOVO

Ni jina ambalo linatumiwa kuita sarafu ya shillingi tano

2.ASHU

Jina linalotumika kuita shillingi kumi

3.MBAO/ MBAULA

Jina hili linaashiria kuwa pesa inayozungumziwa ni shillingi ishirini

4.CHWANI/ HAMSA

Linatumika kumaanisha pesa  inayozungumziwa ni noti ya shillingi hamsini.

5.SOO/ KIOO/ OOS

Ni jina linaloashiria kuwa pesa inayotumika katika mjadala ni shilingi mia moja.

Vile vile jina hilo laweza kutumika katika pesa zingine kwa mfano shillingi mia mbili huitwa "soo mbili", shillingi mia nne litaitwa "soo nne",

Shillingi mia nane huitwa "soo nane" na kadhalika.

6. PUNCH/ SOO TANO

Jina "Punch" ambalo linamaanisha ngumi kwa lugha ya kiswahili, inatumika kumaanisha ni shillingi mia tano.

Ngumi ambayo ina vidole tano mkononi, linaashiria kuwa kila kidole ni mia moja kwa hivo zikiwa tano ni mia tano, hivo basi jina "soo tano"

7.THAO/ NGIRI/ NDOVU

Ni jina ambalo linatumika kumaanisha pesa  ni shillingi elfu moja.

Aidha, shillingi elfu mbili ni  "thao/ ngiri mbili",

Shillingi elfu tano ni "thao/ ngiri tano",

Shillingi elfu nane ni "thao/ ngiri nane", na kadhalika.