Je, unafahamu majina yaliyobandikwa kinara wa ODM Raila Odinga?

Kinara wa ODM Raila Odinga ni mwanasiasa ambaye ameweza kutajika sana katika siasa za humu nchini kwa muda wa takriban miaka 40 sasa.

Raila ambaye ni mwanawe mmoja wa waanzilishi wa taifa hili marehemu Jaramogi Oginga Odinga, alifuata nyayo ya babake na ndiposa amepata kubobea sana katika siasa ya Kenya huku akiwa na wafuasi wengi.

Kwa muda huo wote, wafuasi wa Raila wameweza kumbandika majina kadhaa ambayo wafuasi hao wanahisi kuwa majina hayo yanamfaa kama kiongozi wao.

Haya ni baadhi ya majina hayo:

1.Agwambo.

Raila alibandikwa jina hili mwaka 2007 wakati nchi hii ilkuwa inajiandaa kufanya uchaguzi wa kumchagua Rais na viongozi wengine kabla ya katiba kubadilishwa mwaka wa 2010

2.Baba.

Ni jina ambalo linamaanisha mzazi wa kiume, hivo basi wafuasi wake Raila wana uzoefu wa kumuita baba, kumaanisha kuwa ni yeye wanategemea na vile vile ni yeye kiongozi wao.

3.Tinga

Jina hili linamaanisha mashine ambalo linatumika kulima manake lina nguvu la kufanya kazi hilo.

Raila alibandikwa jina tinga kwani wafuasi wake wanaamini kuwa ana uwezo wa kuwasaidia na kuleta mabadiliko wakati wowote ule wanapomhitaji.

4.Joshua

Jina hili alibandikwa mnamo mwaka wa 2017 je-wafahamu-majina-aliyobandikwa-railawakati uchaguzi mkuu ulikuwa unafanyika, hii ni baada ya Raila kuwaahidi wafuasi wake kuwa atahakikisha kuwa amewafikisha Canaan, ndiposa akapewa jina hilo Joshua.