Je, unakubaliana na Bahati kumhusu Willy Paul?

Staa wa muziki wa injili nchini Bahati ameonekana kumjali na kuwa miongoni mwa watu ambao wanamwombea Willy Paul kujirudi na kuwa na mienendo ya kanisani.

Msanii Bahati ambaye anafanya vizuri na nyimbo inayofamika kama Nyota ametoa kauli yake kumhusu Pozze.

"Namuombea sana.Ni ndugu yangu na maandiko yanasema kuwa hakuna anayeweza akachukua kilicho mikononi mwake mungu. Atarudi tu." alisema Bahati.

Pata hadithi hapa:

Bahati alizungumza haya baada ya picha zilizogaa mitandaoni zikimwonyesha staa Pozze akiwa katika mapozi tata na muimbaji wa Tanzania Nandy.

Wakenya katika mitandao ya kijamii pia walitoa maoni yao kumkaripia msanii huyu ajirudi na kufanya matendo yanayokwenda freshi na kanisa.

Viongozi wa siasa akiwemo Musalia Mudavadi alionekana zaidi kukerwa na picha hizo na video zilizotambaa baada ya fiesta ya Choma Na Ngoma. 

Soma hapa:

Alaine aliyewahi kufanya ngoma na Willy Paul alitokea na kuzima povu ya wakenya kwake Pozze na kuhimiza mashabiki wafanye hivyo kwa upendo mkubwa ila sio kwa kumfokea.

Kumekuwepo na madai kuwa wasanii wa muziki huu wa injili wamebadilika na kuonekana ata kufanya collabo na wasanii wa muziki wa kidunia. Katika mahojiano Msanii Bahati aliwahi kunukuliwa akisema kuwa kwa kufanya nyimbo na wasanii wa nyimbo za kidunia ni njia moja ya kusambaza injili ya Yesu kwa wafuasi wa wasanii hao na dunia mzima.