Je, ushawahi jiuliza ni nani huyu “kijana fupi round”?

Ucheshi wa “kijana fupi round” umeteka anga za ucheshi kwa takriban mwezi mmoja sasa.

Tamko hili ambalo limewafanya wakenya kulifurahia katika mitandao ya kijamii lilifanyika wakati na ambapo gavana wa kaunti wa Pokot Magharibi mheshimiwa  John Lonyangapuo alikuwa akihutubia wananchi na kuonekana kupandwa na mori sana.

Gavana huyu alionekana kugadhabishwa na mwanasiasa aliyegombea kiti cha mwakilishi wodi na kupoteza kwa mpinzani wake wa karibu. Katika hotuba hiyo gavana huyu anadai kuwa mwanasiasa huyu alipata kura tatu na kuaibisha chama chake cha KANU.

Gavana huyu alikuwa anamtupia vijembe mwanasiasa katika kaunti yake anayefahamika kama Dennis Ruto. Mwanasiasa huyu ni katika ya watu wanaopinga uchaguzi wake gavana John.

Ruto alitaka kujua na kuelezwa sababu zinazomfanya naibu wa gavana kaunti hiyo kuwahudumia wananchi akiwa nchi za ng’ambo Marekani badala ya kuwahudumia watu akiwa nchini.

Tamko la gavana huyu linaonekana kutamba kwa kasi sana na kukamata hisia za wengi huku Rais Uhuru Kenyatta akiwa miongoni mwa wakenya wanaofurahishwa sana na jinsi ucheshi huu unavyotokea. Wawili hawa walikutana hapo jana kipindi na ambapo Rais alikuwa ameenda kumfariji aliyekuwa rais wa Kenya mzee Moi kwa kumpoteza mwanawe Jonathan.

Denis Ruto ambaye ameanzisha vuguvugu la kumpinga Lonyangapuo linalokwenda kwa jina Mulmwas katika mahojiano na vyombo vya habari  anadokeza kuwa alihisi vibaya sana aliposikia kwa mara ya kwanza.

Ruto aligombea kiti cha mwakilishi wa wodi ya Lelan katika mkoa wa Pokot Kusini na tikiti ya chama cha KANU  na kupoteza kwa mpinzani  wake Johnson Lokato .