Je Ushawahi Patikana Na Mtoto Ukiwa Mombasa Raha? Getrude Mungai Ana Mawaidha

gertrude mungai
gertrude mungai
Juma hili, mtaalamu wa maswala ya ndoa na ngono, Bi. Gertrude Mungai pamoja na mtangazaji Annita Raey walikuwa wanazungumzia jinsi wazazi wanavyofaa kuweka mikakati kwa nyumba zao wakati wanapoelekea Mombasa raha.

Kulingana na Gertrude, mikakati aliyoweka kwake nyumbani ni ya kuwafunza watoto wake jinsi ya kuwa na nidhamu inapofika wakati wa kulala. Isitoshe wafanyikazi wake wajua kuwa hawapaswi kwenda katika chumba cha watoto kabla yeye na bwanake kuamka.

"Mimi sijawahi shikwa thank God. Shida kubwa ni wafanyikazi kwangu. Mimi hulala nikiwa nimechelewa na asubuhi utapata wasichana wa kazi wamepanda vyumbani vya watoto wetu. Mimi huwaambia as long as mimi na bwanangu hatujashuka chini wasiingie mle. Haya, watoto nao tuna tabia ya kuwapa busu wakilala na hawaruhusiwi kushuka kitandani na kama wanataka kushuka wapige nduru manake sitaki kushikwa nikiwa Mombasa raha." Alieleza Gertrude Mungai.

Baada ya mawaidha yale, waskilizaji wa Radio Jambo walisimulia visa ambavyo vimewakumba wakati wanapoelekea Mombasa raha.

Mtoto wetu wa miaka tisa alinipata nikiwa mechi. Sasa nikamtuma switi dukani na najua mda anaotumia kwa njia kwenda na kurudi.

Lakini sasa huyo mtoto alienda akikimbia na akarudi akikimbia na bahati mbaya akapata tukiwa kwa shughuli.

Sasa alipotupata tulijifanya twacheza na mambo ikawa sawa. Mmoja wao alielezea.

Mwingine naye alisimulia, huo wakati nilikuwa nimekodisha chumba kimoja na tulikuwa tumegawanisha tu na pazia.

Sasa ile masaa tumeingia Mombasa raha tulishtukiwa kijanaa ameingia na akaruka juu yetu.

Sikuzungumza lakini baadaye niliketi naye chini na nikampa mashauri kwani ni wa umri wa mika kumi.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be