Je, Willy Paul kamkosea mungu? Wakenya watoa maoni

Baada ya  mkali wa nyimbo za injili Willy Paul na staa wa kike Nandy kuhusika katika tukio la ajali Mikumi, mkoa wa Morogoro nchi jirani ya Tanzania, wakenya katika mitandao ya kijamii wamepata fursa ya kuzungumza mengi.

Idadi kubwa ya wakenya katika mtandao wa Facebook wakionyesha kutamaushwa na tabia zake Msanii Willy Paul.

Soma hapa:

Willy Paul ni msanii wa nyimbo za kumtukuza mungu. Jamii inamtazama awe katika njia na tabia zinazoendana na kanisa na kumcha mungu.

Vitendo na maneno anayoyasema kulingana na wengi haviambatani na itikadi za dini Picha zilizozagaa mitandaoni baada ya fiesta ya Choma Na Ngoma zinawonyesha katika pozi za kutatanisha na mrembo Nandy.

Katika nyimbo waliofanya pamoja, wawili hawa wanaonekana wakisowera na kupiga maungo ya kimahaba. Willy haoni kuna tatizo kuzichapisha katika mitandao ya kijamii.

Pata uhondo hapa:

Baadhi ya wakenya wanateta kuwa msanii huyu kabadilika na kuingia katika nyimbo za kidunia. Badala ya kumpa pole za tukio la ajali, watumiaji hawa wa mitandao wanamchamba staa willy paul kuwa ni kiboko cha mungu amekipata.

Kati ya jumbe kali hazionekani kumlenga Nandy ila msanii huyu wa injili. Tumekusogezea hapa uone baadhi ya maoni: