OUT AND DOWN? Je,Kiunjuri ametolewa kama kafara ama ni onyo?

Mwangi  Kiunjuri  amefutwa kazi kama waziri wa kilimo na kufurushwa kutoka serikali ya rais Uhuru Kenyatta . Kiunjuri anayejitambua kama mwalimu ,mfanyibiashara na mwanasiasa ameonyeshwa mango katika hatua ambayo haijawashangaza wengi hasa baada ya  kujitokeza kama anayelenga kurithi ufalme wa kisiasa wa rais Uhuru Kenyatta katika eneo la Mlima Kenya baada ya uchaguzi mkuu ujao wa 2022 .

Amelaumiwa  kwa msururu wa matatizo yanayowakumba wakulima nchini  na mara kadhaa katika hafla za umma ,rais Uhuru Kenyatta mwenyewe amewahi kumpa onyo kushughulikia kwa haraka matatizo ya wakulima .Licha ya kuwa huenda ameachishwa kazi kwa sababu ya madai ya utepetevu wake ,suala la Kiunjuri kutaka kuhusika pakubwa na mkondo wa siasa za taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao haliwezi kupuuzwa . Katika sekta ya kilimo ambayo rais katika hotuba yake leo ameiangazia pakubwa ,mambo kadhaa yamemzungusha kichwa Kiunjuri . mgogoro wa kila mara wa mahindi ,bei ya chini ya chain a kahawa na lalama za wakulima kuhusu uzalishaji kupindukia wa maziwa na kupunguz abei ya zao hilo ni baadhi ya masuala ambayo waziri huyo wa zamani wa kilimo alishindwa kushughulikia . Baada ya miaka kadhaa ya kuidai serikali ,wakulima wa miwa katika maeneo ya magharibi na Nyanza pia wamemwtika lawama Kiunjuri kwa masaibu wanayopitia . lakini hayo ya utendakazi wake ndio mwanzo wa ngoma .

Kiunjuri alianza kutokwa ‘uvundo’ pindi tu alipofanya wazi nia yake ya kutaka kufanya ushirikiano wa kisiasa na naibu wa rais William Ruto  ambaye kwa hali na mali anajitayarisha vilivyo usiku na mchana kuhakikisha kwamba anachukua usukani baada ya rais Kenyatta . Hata hivyo wawili hao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu kuliko kipindi walichohudumu wote serikalini .Kiunjuri alikuwa miongoni mwa viongozi  walioandaman na Ruto hadi katika mahakama ya ICC  wakati alipofika kwenye mahakama hiyo kujiondolea lawama kuhusiana na ghasia za baada y uchaguzi wa 2007/2008. Ametajwa kama miongoni mwa viongozi kutoka mlima Kenya ambao wamemkaidi rais Kenyatta kuhusu  kujihusisha na siasa  na huenda shoka lake lilikuwa limenolewa mapema kuliko alivyofahamu . Wakati Ruto anapohitaji wingi wa idadi ya viongozi kuandamana naye katika hafla za kuonyesha uthabiti ,Kiunjuri amekuwa mstari wa mbele kujiunga na misafara kama hiyo .

Mbunge huyo wa zamani alijiunga na  baraza la mawaziri mwaka wa 2015 kuchukua nafasi ya Ann Waiguru katika wizara ya Ugatuzi  na baadaye akahamishwa hadi wizara ya Kilimo katika mabadiliko madogo yaliyofanywa na na rais Kenyatta . wakati wa uteuzi wake mwaka wa 2015 alizingatiwa kama mawaziri wanaopendwa na rais Kenyatta kutoka Mlima Kenya . Lakini bahati ilimtoka wakai rais  alipomkosoa mara kadhaa hadharani kuhusu utendakazi wake .Kuwasili kwa ripoti ya BBI pia kulifika na mazito yake na mgawanyiko wa wanasiasa kutoka Mlima Kenya ,ulimfanya Kiunjuri kujipata katika mrengo ambao haukutazama mambo katika macho kama ya rais . Aliongoza mkutano wa viongozi wa Mlima Kenya kwnda Embu ili kujadili ripoti hiyo na kuchukua msima wa pamoja .Hilo halikumfurahisha rais Kenyatta ambaye baadaye aliwajibu kwamba ‘Alifahamu kila jambo na  wasimdhalilishe kwa sababu ya kunyamaza kwake’.

Wadadisi wanasema kuondoka kwake serikalini miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu huenda ni  hatua itakayompa nafasi ya kujitangaza kama chaguo mbadala kwa  Kenyatta na kutoa mwongozi mpya kwa eneo la mlima Kenya au huenda  nyota imezimwa na kimya kitafuata.