Je,ni kipi kinafaa kutolewa bure? Kondomu au kisodo?

  Serikali inafaa kutoa vitambaa vya hedhi bure badala ya kupeana mipira ya kondomu bila malipo.

MCA mteule Florence Oile anasema ingawaje mtu anaweza kuamua kutoshiriki mapenzi ,hedhi kwa wanawake ni kitu  kisichoweza kuepukika .

Kote afrika , maelfu ya wasichana hukosa kwenda shuleni  kwa ajili ya ukosefu wa visodo . kumekuwa na mjadala wa iwapo vitambaa hivyo vinafaa kununuliwa ilhali mipira ya kondomu hutolewa bure kwa umma .

Hata hivyo wanaharakati wa  kupambana na ukimwi wanashikilia kwamba zimwi la ukimwi ni hatari zaidi na kuna haja ya kutoa kondomu bure .Je maoni yako ni yepi? Ni kipi kinachofaa kutolewa bure kati ya kondomu na kisodo ?