Mkuu wa fedha katika kaunti hiyo Dorcas Lekisanyal amesema agavana Moses Lenolkulal ashateuwa kamati ya watu wanane ikiongozwa na Alex Leseketet ili kuangazia maatumizi ya pesa hizo.
Kamishna wa kaunti hiyo John Korir amesema kutakuwepo na kamati nyingine ya kuangazia mipango nyingine tofauti ya kukabiliana na virusi hivyo hatari.
Lekisanyal amesema ununuzi wa mashine ya ICU na kusambaza chakula kwa familia zilizoathirika kutapewa kipaumbele.
“As at now we don’t have ICU beds, we expect to purchase ICU beds, purchase more personal protective gears for health workers, do more on awareness campaigns and an oxygen plant,” alisema .
Ameongezea kuwa mabwawa ya maji yaliyoaharibika katika kaunti hiyo yote yatakarabatiwa ili kuhakikisha kuwa kuna maji ya kutosha katika Samburu Kaskazini, Samburu Mashariki na Samburu ya kati.