Jinamizi jingine kwa taifa! Watu 13 wamefariki kutokana na kipindupindu

Wakati taifa la Kenya linapoendelea na jitihada za kukabiliana na virusi vya Corona, yamkini wakenya 13 kutoka kaunti zilizoko kaskazini mwa taifa wamepoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo.

Akitoa taarifa ya kila siku kwa taifa kuhusiana na virusi vya corona, waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema watu 12 kati ya 13 waliofariki wanatoka katika kaunti za Mandera na Turkana.

Kagwe alisema kuwa miongoni mwa waathiriwa ni watoto wachanga.

Alisema kufikia sasa watu 550 kutoka maeneo hayo wameathirika na ugonjwa huo na kuongeza kuwa serikali itafanikisha shughuli ya kuwapa matibabu waathiriwa.

Taarifa hizo zinajiri huku kukiripotiwa kuwa wakenya wengine 237 kufikia sasa wamepoteza maisha yao kutokana na mafuriko yanayishuhudiwa katika maeneo tofauti.