Jinsi dhoruba kali ni kero kwa juhudi za uokoaji Likoni feri, lalama za wanamaji

Vikosi vya wanamaji jana vimeshindwa katika zoezi la kutoa gari la Mariam Kighenda na mtoto wake Amanda Mutheu.

Vikosi hivi vinasema dhoruba kali ndo sababu kuu inayochangia zoezi hili kuwa na changamoto.

Hii ni baada ya picha za kamera za majini kuonyesha lililopo gari hilo lenye namba ya usajili KCB 289C .

Kamera za CCTV za feri zinaonyesha kuwa hilo lilikuwa gari la Mariam lililozama.

Soma hadithi nyingine:

Asasi za uokoaji na vyanzo mbalimbali vimeripoti kuwa gari hilo lilipigwa na dhoruba kali na kusogea mbali na walipokuwa wanaitafuta.

Gari hii haijaweza kufikiwa ili kufungiwa nanga zinazoenea juu ya maji ili kusaidia katika juhudi za uokoaji.

Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa serikali Oguna alisisitiza kuwa asilimia kubwa ya mtazamo wa vikosi ni kuwa marehemu Mariam Kighenda na mtoto wake Amanda Mutheu wapo ndani ya gari lao.

Soma hadithi nyingine:

"Gari hilo lilipoonekana na mashine zetu, haikuwa imefungiwa kwa kamba..." Alisimulia mwanamaji.

Zipo taarifa kuwa vikosi vya Afrika Kusini na jeshi la wanamaji nchini haviko sawa katika zoezi hilo.

“Wapiga mbizi wa Afrika kusini wanachukizwa na jinsi jeshi la wanamaji linaendesha shughuli. Wanahisi kwamba wanasukumwa sana ilhali jeshi linafanya juhudi finyu..." kilisimulia chanzo kinachohusika katika zoezi hilo.

Vyanzo vinaripoti kuwa wapiga mbizi wa nchi hiyo ya kusini hawafurahishwi na jinsi jeshi linavyofanya kazi.

Soma hadithi nyingine:

Msemaji wa familia iliyoathirika anasema kuwa matumaini yao yanadidimia zaidi kila uchao.

"Tulijawa na matumaini baada ya taarifa kuwa gari limeonekana na inaonekana inachukua wakati mwingi sana. Tungependa kujua kwa nini haya yanafanyika.