Jinsi jamaa wa miaka 32 alisafiri kutoka Turkana hadi Eastleigh licha ya vizuizi vya polisi

-Rdk9kqTURBXy8yYTM2MDI3ZDE2ZDQ4ZmRlZmEyNDkwMmNlYTYwZDRlOC5qZmlmkpUCzQMUAMLDlQIAzQL4wsOBoTAB
-Rdk9kqTURBXy8yYTM2MDI3ZDE2ZDQ4ZmRlZmEyNDkwMmNlYTYwZDRlOC5qZmlmkpUCzQMUAMLDlQIAzQL4wsOBoTAB
Jamaa, 32, alikamatwa na polisi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kaunti ya Turkana alikuwa amesafiri kutoka kaunti ya Nairobi na kuingia katika eneo la Easleigh licha ya vizuizi vya polisi na hata amri ya kutoingia wala kutoka mtaani Eastleigh.

Huku nchi ikizidi kurekodi visa vipya kila kuchao, wananchi wanaonekana kupuuza amri na maelekezo ya rais na wizara ya afya.

Jamaa huyo aliweza kurudi katika kambi hiyo na dada yake wa miaka 31 na mwanawe, aliyemtoa mjini Eastleigh. Mwanaume huyo wa asili ya kisomali alikamatwa alipokuwa anataka kuingia katika kambi hiyo na jamaa zake.

Maafisa wa afya wa kupima virusi vya corona walisema kuwa mwanaume huyo alipatikana na virusi hivyo na inaaminika kuwa alipata ugonjwa huo katika eneo la Eastleigh.

Naibu gavana wa kaunti hiyo Peter Lotethiro na ambaye ni msimamizi wa maafisa wa afya eneo hilo alisema kuwa jamaa huyo au mkimbizi huyo alitengwa tangu Mei 13.

Inasemekana kuwa jamaa huyo na familia yake walisafiri kutoka Eastleigh hadi kwenya kambi hiyo kwa kutumia texi.

"The taxi driver used the Mai Mahiu route and eventually made it to Lodwar through Eldoret. They entered Turkana through Kainuk, at the border of West Pokot and Turkana, at night.

"On the same night, the taxi travelled to Kakuma and was intercepted at a road block in Lokore, a short distance away from Kakuma town. They were questioned by the security officers and claimed to have taken the child to hospital in Lodwar and Kitale, and were returning home." Alizungumza naibu gavana Peter.

Je, ni nani wamezembea katika kazi yao kwa maana hiki si kisa cha kwanza kuripotiwa jamaa kusafiri kutoka eneo moja hadi lingine, ni swali ambalo linagonga vichwani mwa wananchi wengi.