Jinsi maziwa yalivyochangia Moi kupendwa na watoto

school milk
school milk
Kenya ni jamhuri ambayo imeshuhudia Rais wanne kwa sasa wakitawala nchi hii tokea mwaka wa 1964.

Mzee Jomo Kenyatta ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa jamhuri hii alifanya maendeleo ambayo yaliwapendeza watu ama wana nchi wakati huo.

Viongozi wengine kama vile Rais Mwai Kibaki na Rais wa sasa Uhuru Kenyatta huenda pia walifanya ama walileta maendeleo kadha wa kadha ambayo yaliwanufaisha wazalendo wa Kenya.

Lakini ni vipi Rais wa pili Daniel Moi aliweza kupendwa na watoto wakati alipokuwa mamlakani?

Rais Moi alianzisha kipindi cha kuletea wanafunzi maziwa shuleni. Wakati huo mpango huo ulikuwa unafahamika kama  “MAZIWA YA NYAYO”.

Pindi tu malori yangeonekana karibu na majengo ya shule, kila mwanafunzi alikuwa anajua ni maziwa ya nyayo yameletwa.

Ni kipindi ambacho kilichangia sana vijana wengi kujiunga na taasisi mbali mbali za kusoma kuliko kukaa tu mitaani na kutumia dawa za kulevya. Ni tukio ambalo watoto katika enzi hiyo, hawawezi kumsahau Mzee Moi.

Je, unamkumbuka Rais mstaafu Daniel Moi kwa kufanya nini?