Jinsi msichana alivyozama akijaribu kumwokoa mwanaume aliyekwama majini

Bridge
Bridge
Wanakijiji katika eneo la Ongata Rongai, kaunti ya Kajiado wanaomboleza kifo cha mwanafunzi wa kidato cha 3  aliyezama akijaribu kumwokoa mwanaume aliyekuwa amekwama  kwenye daraja la mto Kandisi.

Anne Nduku mwenye umri wa miaka 19 alizama majini Jumanne katika mto Kandisi akiwa katika harakati za uokozi.

Kulingana na mama yake aliyeshuhudia tukio hilo la mauti, Elizabeth Mutuku alisema kwamba alimwona bintiye akijaribu kujiokoa baada ya kuzidiwa na nguvu ya maji.

Mto huo una daraja ambalo halijakamilika kutengeza  na huwabidi watumizi kusaidiwa na wenzao kuvishwa katika upande wa pili.

"Nilimwona aking'angana sana, hata nikamwita huku nikijaribu kumwokoa lakini juhudi zangu zikaampulia patupu," alisema Elizabeth.

Aidha alisema kuwa alijaribu sana kumwokoa kwa kumrushia kijiti ili nimvute lakini nguvu ya maji ikamzidi na akazombwa na mafuriko hayo.

Kwa sasa mama yake yu ngali anaomboleza kifo cha mwanawe aliyeangamia machoni pake.

Kulingana naye, anasema kwamba ni uchungu sana kumwona mwanawe akifa huku akimwangalia tu bila uzaidizi wowote.

Kulingana na afisa mkuu wa kaunti ndogo ya Kajiado North Joseph Mwika, mwili wa mwanafunzi huyo ulipatikana jioni baada ya kiwango cha maji kupungua.

Anne Nduku alikuwa katika harakati za kumwokoa mwanaume aliyekuwa ameshikilia kwenye daraja baada ya kuzombwa na mafuriko hayo.

Hayo yanatokea huku idara ya hali ya anga ikionya kuhusu ongezeko la kiwango cha mvua wikendi, huku pia ikitoa tahadhari kuwa mvua itaendelea kwa kipindi cha mwezi huu.

Wakenya wameshauriwa kuwa wangalifu mafuriko yanapotokea.

Tahadhari pia imetolewa kwa wale wanaoishi maeneo ya milima kuwa waangalifu dhidi ya maporomoko ya ardhi.

Msemaji wa serikali Cyrus Oguna Jumanne alisema kuwa zaidi ya watu 132 yamefariki kutokana na mvua iliokuwa ikinyesha.

Huku zaidi ya watu 17,000 wakiachwa bila makao