Jinsi punda wanavyo watajirisha wachuuzi wa maji mtaani Rongai, Kajiado

stephen-with-cart
stephen-with-cart
Rongai ni mingoni tu mwa mitaa ambayo imekumbwa na ukosefu wa maji, jambo ambalo limewafanya wakaazi wa eneo hilo kutafuta kila njia ya kupata maji, angalau iwasaidie kwa kufua nguo ama pia kupika.

Ni hali tatanishi kwa wakazi hao ila si kwa wachuuzi wa maji ambao kila siku wanafurahia faida wanayotengeneza kutokana na biashara hiyo.

Wachuuzi hao wanasema kuwa ukosefu wa maji ndani ya mtaa huo umechangia wao kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Punda ambaye ni mnyama wa nyumbani anatumiwa kusafirisha mitungi ya maji nyumba kwa nyumba, huku wachuuzi hao wakisema punda hao wamerahisisha kazi kwani wakipewa chakula na maji, basi kazi yao ni shwari ukilinganisha na kutumia gari ambayo inahitaji mafuta kufanikisha shughli hiyo.