Jinsi ya kuepuka kutongozwa kwenye maeneo ya burudani

burudani (1)
burudani (1)
Baada ya 'mwezi' mzima, wikendi tayari imewadia na kama mwanamke labda unafikiria jinsi ya kutotaka kutongozwa na wanaume kiholela ndani ya maeneo ya burudani.

Ama kwa kweli sio kila mara kama mwanamke unapenda kusumbuliwa kwenye klabu ilhali nia yako ilikuwa kujiburudisha mwenyewe.

Hata hivyo, kama Radio Jambo, tumewaandalia orodha ya jinsi ya kutowavutia au ya kuwaweka mbali wanaume hawa.

  1. Nenda uketi kwenye counter

Counter ni mahala salama sana ambapo waweza keti ndani ya klabu, hii ni kwa sababu hamna viti vya aina ya sofa au viti vilivyo unganishwa. Na hivyo ndivyo utakavyoweza kujivinjari pekee yako.

2. Jinunulie kinywaji chako

Watu wengi hawajui umuhimu au uzuri wa kujibamba pekee yako ndani ya klabu iliyojaa watu aina tofauti.

Kwa hivyo jinunulie kinywaji na sio kinywaji chochote bali kinywaji chenye bei ghali kwani kinywaji ghali kina uwezo wa kuwaogofya kizazi hiki cha kisasa.

3. Piga stori na waiter 

Najua umuhimu wa kuketi kwa counter ni kuepuka wanaume lakini kuzungumza na waiter ni jambo nzuri kwani hata kama unawalenga wengine, yeye ana fursa njema ya kulinda kinywaji chako.

4. Weka sura ya kazi

Mambo ya kuweka sura inayovutia yamepitwa na wakati sasa haswa kwa klabu ambapo unataka kukaa pamoja.

Sura ya kazi itawafukuza wanaume kwani ukitabasamu utaonyesha dalili kuwa ungependa kuwapa mwaliko.

Kunja sura mpaka washtuke.

Muwe na wikendi njema!