Jinsi ya kukabiliana na mtoto wako endapo watarudi shuleni

Siku chache baada ya virusi vya corona kutibitishwa kukita humu nchini shule, makanisa na hata watu walianza kufanya kazi wakiwa nyumba huku rais akiagiza kufungwa kwa maeneo hayo.

Si mmoja au wawili wanafunzi wengi walikatizwa tamaa na virusi hivyo kwa kusalia nyumbani huku wengi wakisahau umuhimu wa elimu na masomo yao katika maisha yao.

Haya basi huku wengi wakitaka shule kufunguliwa na wanafnzi kurudi shuleni,si wote wamo tayari kurudi kwa maana akili zao zishaasahau masomo.

Kama mzazi hizi hapa mbinu za kukabiliana na mtoto wako endapo watarudi shuleni hivi karibuni au mwaka ujao huku tukingoja waziri wa elimu George Magoha kutoa uamuzi wake hii leo.

1.Msikize mwanao

Wakati huu wazazi wengine wanapaswa kuwasikiza watoto wao ambacho wanahitaji na shida ambazo wamepitia kama wanafunzi na haswa kama yuko tayari kurudi shuleni.

Wazazi wanapaswa kutafuta wakati na kuketi na watoto wao na kisha kuwatayarisha kimawazo kuwa wanarudi shuleni na vile wanapaswa kufanya wakiwa na walimu wao.

2.Tambua vichocheo

Kama mzaziunapaswa kufahamu nini kinamfanya mwanao hasirudi shuleni na kutaka kukaa nyumbani haswa nini hicho kinachochea hali hiyo ya kutisha.

3.Msaidie mtoto wako kupumzika

Kwa maana wamekaa nyumbani sana bila ya wengi kushika vitabu wala kupitia vitabu vyao msaidia mwanao kupumzika na kutulia endapo atasikia shule zitafunguliwa.

Wengi hushikwa na kiwewe na hata kusikia kuna msukumo usio wa kawaida katika maishani mwao.

4.Zungumza na mtoto wako na kumueleza hali jinsi ilivyo

Kama mzazi unapaswa kumueleza mtoto wako hali jinsi ilivyo na kumueleza umuhimu wa masomo katika karne hii ya sasa.

Mpe mawaidha mema na kutuliza akili yake, na kisha aweze kutilia maanani elimu na masomo yake.

Asilimia kubwa ya wanafunzi hasa wa darasa la nane na kidato cha nne waliathrika pakubwa kwa maana walikuwa tayari kukabiliana na mtihani wao wa mwisho wa mwaka.