Brothel biz: Jirani yangu anaendelea na biashara yake ya ‘brothel’ licha ya agizo la quarantine

brothel
brothel
Utukutu wa wakenya huanzia utotoni hadi utu uzima na hata katika hali za maisha na kifo, mkenya yungalia hatakuwa mstaarabu wa kujua kizuri na kibaya.

Mwanamke mmoja  amefichua redioni kwamba jirani yake yungali anaendelea na biashara yake ya danguro ambapo wageni wanaingia na kutoka licha ya kuwepo agizo la watu kusalia nyumbani .

Agizo hilo la waziri wa afya Mutahi Kagwe limechukuliwa kama  mchezo na baadhi ya watu ambao wanaendelea kujirundika katika maeneo ya watu wengi.  Siku ya Jumanne, Kagwe alionekana kuhamakishwa na utovu wa nidhamu wa wakenya hasa wazazi ambao wanawaruhusu watoto wao kutangamana katika nyumba za watu binafsi kwa masomo ya ziada baada ya shule kufungwa .

Kando na visa hivyo vinavyojulikana, mpiga simu mmoja wa kike alisema kwamba ameshangazwa na hatua ya jirani yake kuendelea kuwafungulia vyumba watu wanaotaka kulala katika danguro lake .