Jobless:Itumbi apoteza kazi yake katika kitengo cha PSCU

Mwanakimikakati wa mawasiliano ya kidijitali Dennis Itumbi ni miongoni mwa maafisa watano katika kitengo cha mawasiliano ya ris kupoteza kazi zao baada ya tume ya utumishi wa umma kuzifutilia mbali nafasi zao .

Itumbi  alikuwa mkurugenzi mkuu aliyesimamia mawasiliano ya kidijitali .

Nafasi nyingine zilizofutiliwa mbali ni  mkurugenzi mkuu wa mawasiliano anayesimamia  hafla , mkurugenzi mkuu anayesimamia  uandhishi wa hotuba  na afisa mkuu wa mawasiliano .

Nafasi hizo nyingine zilikuwa zikishikiliwa na  James Kinyua, Erick Ng'eno, David  na  John Ndolo. Katika maelezo kumhusu katika twitter ,Itumbi amejieleza kama mfungaji wa nguruwe . Kupoteza kazi yake kumejiri wiki hii ambayo alishehekea siku yake ya kuzaliwa . Itumbi amekuwa katikati ya kesi  inayohusisha barua iliyokuwa na madai ya njama ya kumuua naibu wa rais William Ruto .