Watakaoajiriwa ni walio na stashahada (Diploma) na Astashahada (Certificate).Akilihutubia taifa akiwa Ikuli siku ya jummaosi amesema wafanyikazi hao watahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja .
Amesema shilingi bilioni 1.7 zitatengewa hospitali za umma kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa . rais Uhuru ameongeza kwamba serikali itatenga raslimali zaidi kwa taasisi za utafiti .
"... Ili kufanikisha ubunifu mpya wa kutusaidia kukabiliana na coronavirus’ amesema
Rais Uhuru Kenyatta alikuwa akiratibu mikakati ambayo serikali imechukua ili kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia mpango wa kuzifadhili sekta mbali mbali wakati huu taifa linapokabiliana na janga la virusi vya corona . Wakati wa hotuba yake alitangaza pia kwamba kuna visa vipya 31 vya watu walioambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi hiyo kuwa 1,192.
Wiki jana madaktari walieleza hofu yao ya kucheleweshwa kwa mpango wa kuwaajiri wafanyikazi wa ziada katika sekta ya afya licha ya ongezeko la idadi ya wagonjwa wa Covid 19 .