Joe Kadenge alipenda nambari saba na alifariki Julai 7 - Mwanawe

Siku ya Junatano, wanasiasa, marafiki wa karibu na familia yake Joe Kadenge, walikusanyika kwenye Kanisa la Friends International kumpa heshima zake za mwisho shujaa huyo.

Ilitarajiwa kwamba waombolezi wengi ikiwemo wachezaji wenzake wa zamani wangevaa nguo za jersey lakini walizivaa suti nyeusi. Mjukuu wake peke yake ndiye aliyevaa jersey ya rangi nyekundu na nyeupe.

Kanisa lilikuwa limejaa watu wa kikundi cha umri wake Joe.

Binti yake Esther alisema,

Joe alipenda nambari saba, jeresi yake ilikuwa namba saba, gari yake ilikuwa na nambari saba, namba yake ya nyumba pia ilikuwa ni saba na alifariki tarehe saba ya Julai.

Aliyekuwa dereva wake ndiye aliyetoa hotuba akiwa wa kwanza kwani walienda kila mahali pamoja.

Hakuna mtu mwingine Mzee alipenda kama mimi. Kazi yangu ilikuwa moja na ambayo niliyofurahia kufanya kwani nilikuwa nampelekea maji na kurudisha mkono kwa mtu aliyenichunga vizuri. Nimepoteza rafiki, baba, lakini Mungu alimpenda zaidi.

Ilikuwa furaha kwani familia na wachezaji wenzake walikuja kwa idadi kubwa kusherehekea maisha mazuri aliyoishi. JJ Masika aliwaongoza watu wachache ambao walicheza na Kadenge katika mazungumzo machache.

"Alikuwa shujaa ambaye mimi bado namheshimu. Alikuwa mchezaji mzuri."

Ndugu yake John Anzrah alitoa hotuba ya furaha.

Alikuja nyumbani kutoka Nairobi na kuleta soseji na kutufanya kuwa familia ya kwanza kula soseji katika kijiji chetu.

Mke wake wa pili Mariah Kadenge alikuwa na hisia nyingi na alishindwa kusoma hotuba yake lakini dada zake walisoma kwa niaba yake.

Soma mengi