Sabina Chege

Sabina Chege denies that she was De’ Mathew’s lover

Mwakilisi wa wanawake katika kaunti ya Murang’a Sabina Chege alipuuzilia mbali uvumi kwamba alipata mtoto na sogora wa mziki marehemu John De Mathew.

Alieleza kuhusu uvumi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamziki huyo.

“Sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na John De mathew. Tafadhali heshimu familia yangu na watoto wangu,” alisema wakati akihutubia waombolezaji katika shule ya msingi ya Githambia eneo la Gatanga.

Akiongeza,

Nyinyi ambao mnasema nilipata mtoto na De Mathew si mngemuona leo hapa. 

Sabina aliendelea kuwata wadaku kumheshimu pia.

Mbali na kuwa katika siasa mimi pia ni mama na nahitaji kuheshimiwa.

Sabina Chege
Sabina Chege

Sabina alihusishwa katika video moja De Mathew Njata Yakwa (Nyota yangu) kama mpenzi wake na akaeleza vile walikutana.

Nilikuwa msanii katika kipindi cha televisheni Tausi, (kilichovuma sana nchini miaka ya 90), na huo ndio wakati nilikutana na John De Mathew, nilikuwa mzalishaji wa wimbo wake wa kwanza.

 

Read here for more

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments