John De' Mathew

Mjane wa kwanza wa John D’Mathew Sabina amfariji mke mwenza

 

John D’Mathew alimiminiwa sifa kedekede katika wasifu uliotolewa siku ya Jumamosi wakati wa mazishi yake na familia na marafiki.

Msanii huyo ambaye alitoa jumla ya nyimbo 375 na albamu 50 alichangia sana katika kuimarisha sekta ya mziki nchini.

Akitoa wasifu wa bwanake, Sabina Wairimu Mwangi, mke wa kwanza wa John alisema,

 

John na mimi tulikuwa na fursa ya kuwa wapenzi. Nilikuwa mshiriki na rafikiye. Ulikuwa mwanamume bora na mkarimu.

Ulikuwa kipenzi cha moyo wangu, yule aliyefanya kila jambo kutukinga mimi na watoto wetu. Ulikuwa mtu wa watu na shujaa kwa wale waliokujua. Mwanamume aliyependa bila kushurutishwa na aliyetowa bila kuangalia nyuma.

 

Ulikuwa mtu wa familia na ulifahamu ukweli wa ndoa. Maisha yako yamenifunza kupenda bila masharti na kifo chake kimenifunza kuwa mkarimu na umuhimu wa ukarimu.

 

Nashukuru Mungu kwa fursa ya kuwa na wewe. Utasalia moyoni mwangu.

Kabla ya kumwachia mke mwenza wake Caroline kutoka wasivu wake, alimwambia,

Nakusihi leo tusiruhusu mtu yeyote kuja kugawanya familia yetu. Sisi ni wanyenyekevu, tuna umoja kama familia na hakuna siku tumegombana. Caroline ananiheshimu na hatukaki mtu yeyote kuja kati yetu. 

 

Watoto wetu wanaishi pamoja kwa amani na kama familia moja.

“I really love Caroline because she respects me as Mam Shiko because she knows nilikuwa nimemtengenezea mzee. Those talking bad about Caroline, please respect her. Tutajenga mahali John ameacha na kusikuje mwengine wa kutenganisha watoto. These kids are united as one.

Cariline usiliye, niko hapa. Nitajaza pengo la D’Mathew na kutekeleza majukumu yake.

 

Read here for more

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments