maxresdefault__1577868260_47063

John Pombe Magufuli ampigia simu Diamond Platnumz stejini, amsifia sana

Rais wa nchi jirani ya Tanzania John Pombe Magufuli amefanya tukio la ajabu la kumpigia simu staa mkubwa Diamond Platnumz kipindi na ambapo alikuwa akitumbuiza stejini.

Katika tamasha kubwa lililofanyika Kigoma, msanii huyu alikuwa anasherehekea maadhimisho ya miaka 10 katika sanaa ya muziki.

Rais huyu alifanya kitendo cha mapenzi makubwa kwa msanii huyu.

Magufuli alipiga simu kupitia msemaji wa Chama Cha Mapinduzi Bwana Humphrey na kumsifia kuwa yeye ni mwanaume.

Orodha: Tazama mastaa wanaoishi chumba kimoja bila kuoana

Umati mkubwa wa mashabiki ulijaza ukumbi kwa Kigoma kumpokea staa wa muziki Diamond Platnumz.

Msanii wa kizazi kipya na mkurugenzi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz alifanya bonge la tamasha mjini Kigoma ili kuadhimisha miaka 10 ya uchapakazi katika tasnia ya muziki.

Image result for diamond magufuli

Sherehe hii ilifanyika kwao Kigoma na aliweza kuwaalika mastaa wengi ili kuwapa burudani tele.

Safari ya muziki ya nyota huyu wa bongo fleva ilianza mwaka wa 2009 na kufikia sasa amepiga hatua kubwa pamoja na kuupeleka muziki wa afrika mashariki katika upeo wa juu zaidi.

Miyeyusho ya insta! Willy Paul ampiga kijembe shabiki

Diamond ameweza kutoa mchango mkubwa katika jamii huku akiwatoa kimuziki mastaa kama Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Mbosso pamoja na Lavalava.

Kando na mchango huo wa kupigiwa mfano , Diamond ametengeneza ajira kwa wanahabari kwa kuanzisha kituo cha redio na runinga Wasafi FM na Wasafi TV mtawalia.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments