Joho alifadhili sh1.3m kwa wimbo wa Susumila na Mbosso

susumila
susumila

Msanii Susumila anasema kuwa rafikiye ambaye ni gavana wa Mombasa Hassan Joho alifadhili wimbo wake wa 'Sonona' aliomshirikisha msanii kutoka Tanzania, Mbosso.

Katika mahojiano yetu  Susumila alisema, "The project was like Sh1.3 million and Joho funded all of it. Music production is expensive."

Alisema kuwa 'Sonona' inamaanisha kusononeka "Like you want something but you can't have it. We shot the video in Dar es salaam," alisema.

Awali, gavana huyo alifadhili wimbo wake wa 'Warembo' aliomshirikisha Lava Lava, lakini Susumila anasema kampuni ya kurekodi, 001 Music haimilikiwa na Joho.

"It is a record label founded by myself and three other people, it's a partnership. Joho does not own any record label," alisema.

Msanii huyo wa wimbo wa 'Ngoma Itambe' anasema amekuwa katika urafiki na Joho kwa zaidi ya miaka 15 years.

"We are friends and he knows my potential and that's why he supports me. I have been with him since 2,005 when he was campaigning for a Member of Parliament seat," alisema.

"I'm a loyal friend and I don't campaign for anyone other than him. I believe in him and I believe in his ideologies."

Anasema kuwa yeye na Mbosso walikutana Mombasa, ambapo alikuwa akiwatumbuiza mashabiki wake.

"He came to a show and Joho asked me to talk to him so we can do something together. It was easy working with Mbosso but also hard for me to fit into the Bongo vibe cause I'm used to a whole different thing," Susumila alifichua.

"When we arrived in Dar, It was raining for the three days that we were there."

Susumila ana nyimbo kadhaa na wasanii kama Ommy Dimpoz, Nandy, Redsan na Fally Ipupa. Anawaambia mashabiki wake wangoje ngoma kadhaa kutoka kwake huku akiwashukuru kwa kumshika mkono.