Msanii Willy Paul maajuzi ameteka mitando ya kijamii akiwataka wakenya kumsaidia afikishe ujumbe wake wa msanii wa Jamaica Alaine ili warudiane kama wapenzi .wengi waliamini kwamba ni ilikuwa ukweli Pozze alikuwa akitaka uhusiano wa kimapenzi na Alaine .
Lakini imebainika kwamba zote hizo zilikuwa sarakasi za kutaka kuuangazia wimbo wao mpya na Alaine kwa jina ‘shado Mado’. Wimbo wenye mshiko mzuri huenda utatamba endapo Willy Paul atafaulu kuutangaza vyema mitandaoni na katika mahojiano.
Baada ya wimbo huwekwa youtube mapema ijumaa ,wengi walionekana kumkashifu Pozze kwa kuwachezea shere kuhusu maandishi yake mtandaoi akidai kwamba Alaine hakuwa akizungumza naye kwa sababu ya uhusiano wake na staa mwingine za Bongo Nandy .