download (1)

Jombi ahofia usalama wake baada ya kuchepuka na bibi ya ndugu mdogo

Jacob alipiga simu katika kipindi cha Patanisho ili asaidiwe na watangazaji wa kipindi hicho Gidi na Ghost ili aweze kupatana na ndugu yake mdogo. W

awili hawa wamekuwa hawapatani baada ya Jacob kumwendea kinyume na kuwa mara kwa mara anachepuka na bibi yake. Kisa hiki kilifanyika jumamosi ya wiki jana.

“Ndugu yangu nilikuwa namuibia bibi yake. Sasa nilikuwa nanyemelea bibi ya ndugu yangu mdogo.Nimekuwa nikinyemelea kama mwaka mmoja. Unajua yeye ni mtu wa masafari. Bibi yake aliniambia jamaa hayuko karibu anasafiri  Mombasa.”

Soma mengine hapa:

Noisy couple screaming in lodging skip court date

 Habari za Peter kusafiri Mombasa zilipokelewa kwa shangwe na wawili hawa kwani wangepanga kutoka kwenye klabu na kujivinjari. Siri hii ya mwaka mmoja ilitoboka wakati Peter nduguye aliamua kwenda safari ya Mombasa.  Jacob alijua mdogo wake huwa katika safari za kila siku kwa hivyo akapanga na mkewe wafike klabu kulewa pombe na kujivinjari kama desturi.

“Tulikuwa tumetokea kunywa mbili tatu. Mimi niliskia mtu akikuja na akatupiga makofi na kuniuliza mbona namfanyia hivo.”

Peter alipigiwa simu na msamaria mwema aliyewaona wawili hawa na kumtaka afike klabu ajionee hali halisi ya mambo.

Ilibidi akaikatisha safari yake ya kwenda mombasa.  Alifika kwa hasira na kuwapiga makofi baadae, huku watu wakipata kuona sinema ya mchana. Baadaye alimchukua mkewe wakaenda nyumbani ili kujiepusha na aibu.

Soma hapa:

Patanisho: Bibi amtoroka bwanake baada ya kuuza shamba

Sasa Jacob anasema kuwa maisha yake yamo hatarini kwani Peter anapendekeza wakutane nyumbani katika kikao ili wazime tofauti zao na kujadili swala nzima mwanzo mwisho. Kikao hiki kinapendekezwa kifanyike nyumbani kwa  baba yao na ndugu mkubwa ambaye ni mwanapolisi.

Kulingana na Jacob huenda akapata kichapo kikubwa kutoka kwa ndugu yao mkubwa. Anataka waweze kusameheana kabla kikao hicho kufanyika

Alipopigiwaa simu na Gidi, Peter alieleza kwa machungu jinsi alivyojitolea kumpeleka shuleni bibi yake, baadae akapata ajira. Anasimulia jinsi amekuwa akiacha watoto na upweke na kuenda kulewa na ndugu yake mkubwa

Amekuambia makosa yake? Unajua kama sio nyinyi singeshika simu. Huwa naskia umbeya nasema kuwa hawezi fanya fanya hivo na bibi yangu. Nimesomesha bibi mpaka akaingia kazini halafu akuje kumnyemelea. Huyo mtu amenichezea kwa miaka mingi.  Imagine wanaacha watoto na kuenda klabu,” alihadithia Peter.

Wawili hawa walisameheana na kupanga wakutane nyumbani ili kumaliza kabisa tofauti zao.

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments