Soma hapa:
Bibiye jamaa huyu alikuwa anapata ubuyu kuhusu jinsi bwanake anavyochepuka na binti fulani ofisini. Kando na cheche za ubuyu wa majirani, bibiye alianza kuona mabadiliko ya tabia ya bwanake kama kuja nyumbani masaa ya usiku na wakati mwingine kukesha nje na kuja nyumbani siku inayofuata.
"Tulikuwa na mzozano na bwanangu kuhusu yeye kuja nyumbani kama amechelewa. Alianza kuchelewa sio kama awali. Iwapo angechelewa angepiga simu na kunieleza." alifunguka bibiye.
Bibiye alijanjaruka na kujua atamwendea kwa mganga ampe dawa mujarabu ya kumnasa bwanake.Dawa hii ilifanya kazi kwani baada ya siku mbili alipigiwa simu na watu walioshuhudia kisa hiki mubashara.
Pata uhondo hapa;
Bwanake aliomba msamaha na kusema kuwa atamfuta kazi katibu huyo na baadaye bibiye akapigia daktari wake wa mitishamba na kumwambia jinsi atakavyowafanya huru.
"Daktari wangu alisema niwamwangie dawa fulani alikuwa amenipa na wakawa sawa." alisimulia mkewe.